The House of Favourite Newspapers

Mambo Matatu Yanayomkera Shehe Mkuu Mwezi Mtukufu

0

AlhadiMussaSalumShehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salim.

Na Mwandishi Wetu, UWAZI

DAR ES SALAAM: Mwezi Mtukufu wa Ramadhan umewadia na leo ni Chungu cha Kwanza, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salim amesema kuna mambo matatu anayoyachukia au kumkera kwenye kipindi hiki.

Akizungumza kupitia runinga moja jijini Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita, shehe huyo alisema kuwa, mara nyingi Ramadhan inapoingia, kuna baadhi ya Waislam hufanya maasi wakisema ya mwishomwisho na kuyaita vunja jungu jambo ambalo ni kinyume na Kurani.

Alisema: “Kwa kweli kuna mambo matatu huwa siyapendi kabisa wakati wa kukaribia mfungo wa ndani ya mfungo wenyewe.

“Kwanza ni wale watu wanaofanya maasi halafu wanasema wanavunja jungu ili kuingia kwenye mfungo. Pia, kuna wale wanaojisingizia maradhi wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ili wasifunge. Hii si sawa hata kidogo.

“Lakini jambo la tatu ni wale wanaohamia nchi nyingine. Kuna watu wakati wa kufunga wanahamia kwenye nchi nyingine ili kukwepa funga. Haya ni mambo matatu ambayo yananikera sana.”

Kutoka Dawati la Uwazi

Mhariri na waandishi wake, wanawatakia Waislam wote nchini na duniani mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Leave A Reply