The House of Favourite Newspapers

Man United Yaichakaza Arsenal

0

Mashetani Wekundu, Manchester United wameibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England katika Uwanja wa Old Trafford.

 

Mabao ya Manchester United yamefungwa na Wareno, Bruno Fernandes dakika ya 44 na Cristiano Ronaldo mawili dakika ya 52 akimalizia pasi ya Marcus Rashford na 70 kwa penalti baada ya Martin Odegaard kumuangusha Fred.

 

Mabao ya Arsenal yamefungwa na Emile Smith Rowe dakika ya 13 akimalizia pasi ya Mohamed Elneny na Martin Odegaard dakika ya 54 akimalizia pasi ya Gabriel Martinelli.

 

Kwa ushindi huo mbele ya kocha mpya mtarajiwa, Ralf Rangnick, Manchester United inafikisha pointi 21 na kusogea nafasi ya saba, wakati Arsenal inabaki na pointi zake 23 katika nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 14.

Wakati huo huo, Michael Carrick aliyekuwa kaimu kocha wa Man United baada ya kufukuzwa Ole Gunnar Solskjaer naye aliachia ngazi rasmi baada ya ushindi huo tayari kumuachia jukumu Ralf Rangnick.

 

Carrick amekuwa na klabu hiyo tangu mwaka 2006 alipowasili kama mchezaji kutoka Tottenham Hotspuras na katika kipindi chake akisukuma kandanda ameichezea mechi 464 Manchester United na kushinda mataji matano ya Ligi Kuu ya England, moja la Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA.

 

Kama Kocha Carrick ameiongoza Man United michezo mitatu akishinda miwili na kutoa sare mchezo mmoja.

Leave A Reply