The House of Favourite Newspapers

Zari Akana Kumpa Penzi Diamond Tangu Waachane

0

MWANAMAMA tajiri Afrika Mashariki mwenye maskani yake Afrika Kusini, Zari The Boss Lady amekana kumpa penzi mzazi mwenzake, Diamond Platnumz tangu walipoachana siku ile ya Februari 14, 2018 (Valentine’s Day).

Ingawa wameonekana pamoja mara kadhaa, Zari anasema yote ni kuhusu malezi ya pamoja (co-parenting) ya watoto wao wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan.

Akizungumza kupitia chaneli yake ya Mtandao wa YouTube ya The Hassan’s, Zari anasema; “Uzazi wenza umekuwa rahisi kwani tuliamua kuweka hisia zetu kando, sijawahi kuwa na mahusiano naye ya kimapenzi baada ya kuachana.

“Wakati mwingine watoto wanafikiri tumetengeneza, lakini hatujafanya hivyo. Hii ni kwa sababu mara chache Diamond ametutembelea.

“Kama vile tulipokuwa tukirekodi Netflix alikuja Afrika Kusini. Ikiwa yuko chumbani mwangu, mimi huwa natoka chumbani. Lakini sisi bado ni marafiki wazuri.”

Leave A Reply