The House of Favourite Newspapers

Manji Akamatwa Tena Wakati Akitoka Sentro, Arudishwa Ndani

MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga na Diwani wa Kata ya Mbagala,  Yusuf  Manji leo amefikakatika Kituo Kikuu cha Polisi Dar,  kama alivyoahidi jana baada ya kutajwa kwenye orodha ya watu 65 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Yusuph Manji alifika asubuhi kwenye kituo cha Polisi cha kati ambapo baadaye alionekana akiwa anatoka nje ya kituo  kuondoka lakini ghafla akazuiwa na Polisi na kumwambia anahitajika ndani tena. Manji alirudishwa kituoni hapo akiwa tayari amefika nje akiwa tayari kuondoka.

Comments are closed.