The House of Favourite Newspapers

Mapinduzi, Mustapha Wampasua Kichwa Nabi

0

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga, amesema anapenda kuona wachezaji wake wote wakiwa uwanjani, lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake inakuwa ngumu kuwatumia wote.

 

Miongoni mwa wachezaji ambao kwa sasa wapo chini ya uangalizi mkubwa wakiendelea na program ili kurejea uwanjani ni pamoja na Mapinduzi Balama na Yassin Mustapha ambao hawajaonekana uwanjani kwa muda mrefu wakiuguza majeraha.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Nabi alisema: “Wachezaji wa Yanga katika hali ya kawaida wote ni bora na endapo watakuwa vizuri kiafya na utimamu wa mwili basi tutafanya vizuri.

 

“Kikubwa kwa wakati huu ni kuona hali za wachezaji wote zinaimarika kisha hapo tutaona namna kikosi ambavyo kinakuwa imara. Wale ambao walikuwa ni majeruhi ikiwa ni Mapinduzi Balama na Yassin Mustapha, hawa wote ni wachezaji wazuri na wakimaliza program zao itapendeza.”

SALUMU SADIKI NA LILIAN CHULA (TUDARCO)

Leave A Reply