Mashujaa: Tupeni Yanga FA Tuwanyooshe

Kikosi cha Mashujaa FC wanashiriki Ligi Daraja la Kwanza wakiwa kundi B na wana pointi saba.

BAADA ya kuwaondoa Simba katika mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa kwa ushindi wa mabao 3-2, Mashujaa wanatamani kucheza na Yanga. Mashujaa FC wanashiriki Ligi Daraja la Kwanza wakiwa kundi B na wana pointi saba wakiwa wamecheza michezo saba, wameshinda miwili na sare mchezo mmoja na kupoteza michezo minne.

 

Katibu wa Mashujaa FC ya mkoani Kigoma, Khatibu Mtumwa alisema wanaona fahari kuitungua
Simba kibabe hivyo maombi yao kwenye droo ijayo wapangwe na Yanga ama Azam.

” Sasa maombi yetu tupangwe na timu kubwa za Ligi Kuu kama Yanga, Azam, Mtibwa Sugar na Lipuli ili tuwanyooshe vizuri kwa kuwa hesabu zetu ni kupanda daraja hivyo kwa kupata matokeo tunapata mwanga wa kusonga mbele.

 

“Wengi wanasema tumebahatisha hivyo tukifanikiwa kuzitungua timu hizo kubwa zitafanya tuwe na ubora na kuheshimika zaidi tukifanikiwa kupanda Ligi Kuu, tupo tayari na tutavunja rekodi zote zilizowekwa kwa kila tutakayekutana naye,” alisema.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA

Loading...

Toa comment