The House of Favourite Newspapers

Maskini Binti Huyu, Anavaa Pampas Tumboni, Ana Figo 1 Na Mguu Mmoja – Video

0


Msichana mdogo, Husna Saidi Munde, mkazi wa Kawe Kanisani jijini Dar es Salaam, anaishi katika mateso makali baada ya kuzaliwa akiwa hana njia ya haja kubwa na kulazimika kutobolewa ubavuni ambapo hulazimika kuvaa ‘Pampas’ zaidi ya tatu kwa siku na kufunga kitambaa ili kuzuia haja kubwa.

Amesema hana fedha za kununua kifaa maalum kinachoitwa Colostomybag kwa ajili ya kuzuia uchafu.

Akiongea kwa uchungu na Global TV, Husna ambaye pia alizaliwa na tatizo la figo moja kutofanya kazi, amesema hulazimika kwenda kusafishwa damu (Dialysis) mara tatu kwa wiki lakini pia hana mguu mmoja kwani alizaliwa mguu ukiwa umejikunja na mfupi hivyo ukakatwa.

Husna anateseka, kama umeguswa na hali yake, unaweza kumsaidia kwa chochote ili kuokoa maisha yake.

Namba ya msaada: 0719942561, Jina ni Stumai Mwishehe (mama yake mzazi).

Leave A Reply