The House of Favourite Newspapers

MASOGANGE AZIDI ‘KUMTESA’ RAMMY GALIS

KUFUATIA msiba wa msanii Agnes Gerald ‘Masogange’, msanii mwenzake Rammy Galis amekuwa mtu wa huzini, kulia na majonzi mazito hasa wakati anapoona jeneza lenye mwili wa marehemu.

Baada ya mwili wa marehemu kufika nyumbani kwao maeneo ya Utengule, Mbalizi mkoani Mbeya, msanii huyo alionekana kukosa raha na huku wasanii wenzake wakimsihi apunguze mawazo na ajipe moyo hasa katika kipindi hiki cha majonzni.

Rammy ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Masogange, jana alianguka na kuishiwa nguvu wakati akiaga mwili wa marehemu katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita katika kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngomakilichopo Mwenge jijini Dar ambapo jana aliagwa katika Viwanja vya Leaders na kusafirishwa kwenda kwao ambako amezikwa leo.

 
PICHA NA HILALLY DAUDI | GLOBAL TV ONLINE, UTENGULE, MBALIZI, MBEYA

Comments are closed.