The House of Favourite Newspapers

Mau Fundi Awafunga Mdomo Wakongo

0

 

KOMEDIANI matata Bongo, Maulid Fundi almaarufu Mau Fundi amesema amewafunga mdomo waigizaji wa vichekesho wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akiwemo kinara wao wa vichekesho aitwaye Bienvenu Prosper Amani au Jackson kupitia kazi yao inayokwenda kwa jina la Mjomba.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Jackson anasema kuwa, ametoka mbali kwa ajili ya kufanya kazi hivyo Mau Fundi lazima ajipange kwani kwa Bongo atahakikisha anamkalisha kwani anataka kuchanganya ladha kutoka Kongo na Tanzania.

 

“Kufanya kazi na Mau kwangu ni faraja sana na ninajua tutaleta umoja mzuri sana katika kazi na ni kitu ambacho ninapenda, watu wasiache Jumamosi (kesho) kufuatilia kazi yetu ambayo itatoka ya Mjomba,” anasema Jackson.

 

Kwa upande wa Mau anasema kuwa, anachojua yeye amewafunga mdomo Wakongo ndani ya kazi hiyo ya Mjomba.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply