The House of Favourite Newspapers

Mayele: Msiogope, Nawafunga Tena Bamako Uwanja wa Mkapa jijini Dar

0
Mkongomani Fiston Mayele

MSHAMBULIAJI kipenzi cha Wanayanga, Mkongomani Fiston Mayele amewaondoa mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia wasiogope kwenda uwanjani na hawatawaangusha watakaporudiana dhidi ya Real Bamako ya nchini Mali.

Timu hizo zinatarajiwa kuivaana katika mchezo wa raundi ya nne wa hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa leo saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

Katika mchezo uliopita uliopigwa huko Mali, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 huku la Yanga likifungwa na Mayele.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mayele alisema kuwa mbinu na maelekezo ambayo wameyapata kutoka kwa kocha wao Mtunisia, Nasreddine Nabi yanatosha kwao kupata ushindi katika mchezo huo.

Mayele aliongeza kuwa, kwa upande wake atahakikisha anatimiza majukumu yake ya uwanjani ya kufunga na kutengeneza nafasi za kufunga kwa wachezaji wenzake ili kufanikisha malengo yao.

Aliongeza kuwa katika mchezo uliopita walishindwa kupata matokeo mazuri ya ushindi ugenini kutokana na kutowajua vizuri wapinzani pamoja na udogo wa uwanja ambao waliutumia katika mchezo huo.

“Kiufundi uwanjani tuliotumia katika mchezo wa kwanza ugenini huko Mali ulitufanya tushindwe kucheza aina ya soka letu tulilolizoea la mipira mirefu kwenda goli la wapinzani wetu.

“Kwani uwanja huo ulikuwa mdogo, hivyo basi wamekuja kwenye uwanja wetu wa Mkapa, basi niwaondoe hofu kuwa hatutawaacha hapa ni lazima tuwafunge.

“Niwaahidi mashabiki kuwa, tutaingia uwanjani kwa ajili ya kupata ushindi pekee na sio kitu kingine ili tujiweke katika nafasi nzuri nzuri katika msimamo wa kundi letu,” alisema Mayele.

AUCHO YUKO FITI

Naye Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ameliambia Championi Jumatano kuwa: “Khalid Aucho ambaye aliumia katika mchezo wa kwanza naye yupo fiti na atapatikana katika mchezo wetu hivyo hakuna namna nyingine ambayo watapona hwa Real Bamako, mashabiki wanatakiwa waje wakiwa wanajiamini kupata furaha.”

STORI: WILBERT MOLANDI

EXCLUSIVE: RAHISA AFICHUA UJAUZITO wa PATRICK, AANIKA SMS za NIFFER, AMTUMIA SALAMU HIDAYA NJAIDI..

Leave A Reply