The House of Favourite Newspapers

Mayweather Agoma Kupiga Picha na Kijana Aliyepaka Rangi Kucha

0

Hizi hapa ni za kutokea pande za Marekani, ambapo mchezaji wa ngumi za kulipwa duniani Floyd Mayweather  ameonekana akikataa kupiga picha (selfie) na kijana mmoja wa miaka 18 ambaye alikuwa amepaka rangi za kucha.

 

Tukio lilitokea muda mchache baada ya kumalizika kwa mchezo wa kikapu kati ya Grizzlies dhidi ya Clippers uliofanyika katika uwanja wa Staples Center, ambapo kijana huyo alimfuata Myweather kwa ajili ya kupata picha ya pamoja lakini Floyd alipoona rangi katika kucha za kijana huyo alikataa kupiga naye picha.

 

Katika video inayosambaa mitandaoni ,Mayweather alisikika akisema ‘’ You got painted nails, I don’t take pictures with guys with painted nails (Umepaka kucha rangi, huwa sipigi picha na wanaume walipoka kucha zao rangi)”

 

Cc; @bakarimahundu

Leave A Reply