The House of Favourite Newspapers

Mbunge Amkomalia Magufuli Aongezewe Muda Madarakani

0

MBUNGE wa Makambako (CCM), Deo Sanga, jana Jumatano Februari 3, 2021, amerudia kauli yake ya kutaka Rais John Magufuli aongezewe muda wa kukaa madarakani.

 

 

Ameeleza hayo bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa hotuba ya Magufuli ya ufunguzi wa Bunge la 12 aliyoitoa mwishoni mwa mwaka 2020.

 

 

Katika Bunge la 11, Sanga amewahi kueleza jambo hilo zaidi ya mara mbili akitaka kiongozi mkuu huyo wa nchi anayemaliza muda wake wa miaka 10 mwaka 2025, kuongezewa muda ili aendelee kukaa madarakani huku akitaja sababu mbalimbali.

 

 

Mbali na Sanga, mbunge wa zamani wa Chemba (CCM), Juma Nkamia, na aliyekuwa mbunge wa Nkasi Kaskazini kwa tiketi ya chama hicho tawala, Ally Keissy, nao waliwahi kuzungumzia suala la Magufuli kuongezewa muda, kauli ambayo iliungwa mkono na Spika Job Ndugai.

 

 

Hata hivyo, Rais Magufuli amekuwa akikaririwa akisema kuwa hawezi kuongeza muda. Machi mwaka 2020 katika mahojiano maalum na Mwananchi, Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally, alisema Magufuli hana mpango wa kubadilisha katiba ili kuendelea kukaa madarakani kwa awamu ya tatu na wanaosema hilo watafute mtu mwingine wa kufanya hayo.

 

 

“Huyu Magufuli (John) lazima aongezewe muda, atake asitake tumuongezee mbona mataifa mengine kama China walifanya hivyo,” amesema Sanga bungeni jana.

Leave A Reply