The House of Favourite Newspapers

Mchumba wa Diamond ni Huyu

0

KUMEKUWA na mgagaziko kwa muda mrefu tangu staa wa muziki barani Afrika, Nasibu Abdul au Diamond Platnumz atengane na baby mama wake, Tanasha Donna mapema mwanzoni mwa mwaka 2020 ambapo swali zito limekuwa anaminya na nani hasa kimapenzi?

 

Kwa sasa hilo siyo swali tena kwani majibu yamepatikana kwamba, mchumba wa kukata na shoka wa Diamond au Mondi yupo nje ya nchi na si nchi nyingine, bali ni bondeni Afrika Kusini (Sauzi).

 

Hata hivyo kuna wanaodhani ni mwanamama Zari The Boss Lady ambaye amezaa na Diamond watoto wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan na anaishi Sauzi, lakini taarifa ikufikie kwamba, siyo yeye.

 

Juma Lokole ni mtu wa karibu wa familia ya Mondi, hasa Mama Dangote ambaye ndiye ‘last say’ amethibitisha hilo.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA juu ya Mondi kutoonekana na kifaa kipya na kama yupo singo kwa kipindi chote hicho tangu alipoachana na Tanasha, jamaa huyo ametoa ishu ya ndani kuwa ana mchumba ambaye hayupo Bongo.

 

Lokole anasema; “Ni kweli haiwezekani akawa singo tangu kipindi hicho, lakini ukweli ni kwamba mchumba wake yupo nje ya nchi…”

Alipobanwa yupo nchi gani, Lokole anasema; “Yupo Afrika Kusini; ni mtoto f’lani hivi mkali sana.”

 

Alipoambiwa mchumba wa Mondi aliyeko Sauzi ni Zari ambaye ni baby mama wake, Lokole alikataa katakata kwamba, siyo mwanamama Zari.

 

Katika ufukunyuzi wa Gazeti la IJUMAA, ni kweli huwenda Mondi akawa na uhusiano na mrembo wa Sauzi aitwaye Andrea Abrahams ambaye amekuwa akihusishwa naye kwa muda mrefu.

 

Andrea ni bonge la mwanamitindo maarufu wa nchini Afrika Kusini. Mbali na kuwa mwanamitindo, pia anashikilia cheo cha Miss Mamelodi Sundowns Mpumalanga na Miss 7 Continents kwa mwaka 2016.

STORI; KHADIJA BAKARI, DAR

Leave A Reply