The House of Favourite Newspapers

Mdau wa Soka Afunguka, Ammwagia Sifa Ntibazonkiza Adai Yeye ni Kama Mvinyo

0
                                    Kiungo wa Klabu ya Yanga raia wa Burundi Saido Ntibazonkiza

UBORA wa Saido Ntibazonkiza umeendelea kuwa juu tangu sakata lake la utovu wa nidhamu na Klabu ya Yanga kumalizika.

 

Kwa mujibu wa Salehe Ally ‘Jembe’ Mchambuzi wa kipindi cha Krosi Dongo kinachorushwa na Global TV na Global Radio anadai Saido ni kama mvinyo kadri anavyozidi kuzeeka ndivyo anavyozidi kuwa mtamu katika soka

 

Kwa asilimia kubwa mchezo wa jana uliamuliwa na ubora wa Saido maana yeye ndiye mchezaji aliyechezewa faulo nyingi sana lakini pia utimamu wake wa mwili ulikuwa wa hali ya juu hadi kufanikiwa kumaliza dakika zote 90 licha ya kwamba ametoka kuoa hivijuzi tu.

                                                         Saido Ntibazonkiza akiwa ndani ya Uzi wa Yanga

Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa  moja dhidi ya Klabu ya Azam huku mfungaji wao kinara wa mabao Fiston Mayele akifanikiwa kufunga bao la pili na kufikisha idadi ya mabao 11 akiwa kinara katika msimamo wa Wafungaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC mpaka sasa.

Leave A Reply