The House of Favourite Newspapers

Mdee Ashauri Wabunge Wote Wapimwe Corona

0

MBUNGE wa Jimbo la Kawe (Chadema) na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho, Halima Mdee, amelishauri bunge  kuwapima wabunge wote ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 unaosambazwa na virusi vya Corona.

 

Mdee amesema hayo leo Jumanne, Machi 31, 2020,  wakati akitoa hoja kwenye kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa bunge hilo la 11, jijini Dodoma na kuongeza kuwa watakaobainika kuwa na Corona wawekwe karantini, na ambao hawana waendelee kufanya kazi.

 

“Mhe. Spika nilikuwa naomba kupata ufafanuzi kutoka kwako katika kipindi hiki cha bunge, nilidhani ni busara kwa serikali kuja kutoa taarifa kwa Bbunge juu ya hali ya Corona nchini, tulijadili kwa kina na tuangalie mpango wa serikali wa dharura.

 

“Nadhani kama nchi kuna hatua kubwa zinapaswa kuchukuliwa na haiwezekani bila kupata ‘proper report’, tuulize maswali tujibiwe ili tuweze kuokoa wananchi, kama Marekani dunia ya kwanza inatapatapa, Italy na Spain pia, hili jambo ni kubwa.

 

“Tuangalie serikali ina mipango  gani ya dharura ya bajeti…  Wenzetu huko wakisema total isolation au total lockdown ni kwamba serikali inafidia wananchi. Serikali inafidia wafanyabiashara,  kunakuwa na package mahususi unaponiambia Halima nisiende kwenye biashara.  Kama nilikuwa ninapata Tsh 1000 serikali ina-approve hata robo ili niweze kutulia nyumbani,” amesema.

 

Naye Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa akichangia hoja ya  Mdee alisema,  “Hii ni vita ambayo tunatakiwa kushirikiana kwa pamoja kupambana…  tusipokuwa waangalifu inaweza kuanza kumdondosha mmoja-mmoja katikati yetu.”

 

Mpaka jana wagonjwa waliokuwa wameambukizwa virusi vya corona nchini Tanzania walikuwa 19 ambapo leo asubuhi, mgonjwa mmoja amefariki dunia katika kituo cha matibabu ya wagonjwa wa corona katika Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.

 

Leave A Reply