Miguu ya Queen Darleen Gumzo

Mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye pia ni dada wa staa wa muziki nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ hivi karibuni alizua gumzo baada ya kuweka picha ya miguu yake kwenye mtandao wa Instagram.

 

Queen Darleen aliweka picha hiyo kwenye mtandao wa Instagram kupitia Insta story ambapo watu mbalimbali walichukua picha hiyo na kuwa gumzo kila kona kwa kile walichodai kwamba miguu yake inafanana na ya kiume.

 

“Miguu ya kikongwe au, maana hapo Queen hafanyi kazi ngumu. Je, angekuwa na life lakuhustle miguu ingekuwaje, miguu kama gari la site, lile linalotoka feri kwenda dampo chanika,” aliandika mmoja wa mashabiki kwenye mtandao huo.

 

Toa comment