The House of Favourite Newspapers

Mimba kutunga nje ya mfuko wa kizazi- 3

0

hemorrhoids-during-pregnancy.jpgKARIBU msomaji katika makala haya, wiki mbili zilizopita tulikuwa tunaangalia tatizo la mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi. Na tuliangalia maeneo ambayo mimba hizo hutungwa.

Leo ningependa tuangalie sababu za tatizo hili na dalili za mwanamke mwenye tatizo hili.

Nini husababisha mimba kutunga nje ya kizazi?

Katika mimba nyingi zinazotunga nje ya uterus, chanzo chake huwa hakijulikani. Hata hivyo kuna vihatarishi ambavyo humfanya mwanamke kuwa katika hatari ya kupata tatizo hili. Vihatarishi hivi ni pamoja na:

  1. Matatizo katika mirija ya fallopian.

Magonjwa yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja na:

  • Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke (PID).
  • Matumizi ya vitanzi vya kuzuia mimba (Intra-uterine contraceptive devices).
  • Kuoteana kwa tishu za uterus kwenye viungo vingine vya uzazi au endometriosis.
  1. Uvutaji sigara

Uvutaji sigara kwa mwanamke una uhusiano mkubwa na utungaji wa mimba nje ya kizazi. Imeonekana kwamba wanawake wanaopendelea kuvuta sigara mara kwa mara wana hatari ya kupatwa na tatizo hili mara tano zaidi ya wale wasiovuta kabisa. Hali hii husababishwa na ‘nicotine’ iliyomo ndani ya tumbaku. Kwa kawaida nicotine huchochea kusinyaa kwa mirija ya fallopian hali iletayo kuziba kwa mirija hiyo na hivyo kufanya kiinitete kushindwa kupita kwenye mirija kuingia kwenye uterus na kufanya mimba kutunga kwenye mirija ya fallopian.

  1. Upasuaji wa tumbo uliofanyika zamani.

Operesheni yeyote inayohusu mirija ya fallopian inaongeza uwezekano wa mwanamke kutunga mimba nje ya uterus kwa vile mirija ya fallopian huwa imesinyaa kutokana na operesheni hiyo.

  1. Matumizi holela ya baadhi ya dawa.

Matumizi ya baadhi ya dawa zenye homoni husababisha kupungua kwa uwezo wa mirija ya fallopian kusukuma kiinitete kuelekea kwenye uterus na hivyo kuleta uwezekano wa utungaji wa mimba nje ya kizazi. Dawa hizo ni kama dawa za kuzuia mimba zenye homoni za kike za progesterone, na dawa za kusaidia uzazi aina ya clomiphene.

Dalili za ectopic pregnancy

Katika wiki za mwanzo za ujauzito, mimba iliyotunga nje ya uterus huwa na dalili sawa na za mimba ya kawaida. Dalili hizi ni pamoja na mwanamke kukosa hedhi, kujaa kwa matiti, kichefuchefu, na uchovu wa mwili. Hali hii hufanya ugunduzi wa mimba iliyotunga nje ya uterus kuwa mgumu katika hatua zake za awali.

Hata hivyo dalili ya awali ya kuonesha kuwa mimba imetunga nje ya kizazi ni kuwepo kwa maumivu makali na damu kutoka ukeni. Maumivu yanaweza kuwa kwenye nyonga, tumbo au wakati mwingine kwenye mabega au shingo (iwapo kiwango cha damu inayotoka kwenye mirija iliyopasuka ni kingi sana mpaka kugusa kiwambo cha hewa).

Maumivu haya huweza kuwa makali na yanayokata kama kisu, na yanaweza kuwa upande mmoja zaidi wa nyonga ingawa si lazima yawe upande ulio na mimba.

Dalili nyingine

  • Kizunguzungu na kuzimia kwa sababu ya kupoteza damu kwa wingi.
  • Shinikizo la damu kuwa chini.
  • Maumivu ya chini ya mgongo

Kuna njia za kuepuka tatizo hili hivyo ni vema ukafuatilia makala haya nikukumbushe kuwa Sigwa Herbal Clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume unaweza ukawatembelea katika vituo vyao vilivyopo nchi nzima kwa maelezo na msaada usisite kupiga simu.

Leave A Reply