The House of Favourite Newspapers

Mjane wa Kobe Bryant Asitisha Mkataba na Nike

0

Kobe Bryant, aliyekuwa mchezaji kikapu (NBA) maarufu duniani akitokea pande za Marekani alistaafu kikapu mwaka 2016 na kuongeza mkataba wa miaka 5 na kampuni ya Nike wa kuzalisha viatu vyake vinavyojulikana kama Mamba, miaka minne baadaye Kobe alifariki katika ajali ya helikopta akiwa na mtoto wake wa kike aliyekuwa na umri wa miaka 13, marafiki zake sita na rubani wa helikopta hiyo, Januari 26, 2020.

 

Siku za hivi karibuni mjane wa Kobe Bryant, Vanessa Marie Bryant ameonesha nia ya kutoendelea tena na kampuni ya NIKE katika kuzalisha bidhaa zote zenye nembo ya Kobe Bryant (KB24), kwa kile alichokiita ni kulinda heshima na urithi wa Kobe Bryant.

 

Vanessa hakuwa tayari kuweka sahihi mkataba kati ya NIKE na Kobe Bryant uliodumu kwa miaka 18, huku akiituhumu kampuni hiyo kwa kuzalisha viatu vya kumuhenzi mtoto wake Gianna aliyefariki katika ajali ya helikopta akiwa na baba yake (Kobe Bryant) bila ya kushirikishwa.

 

Vanessa alianza kuonesha nia ya kutoendelea na ushirikiano wa kibiashara na Kampuni ya NIKE tangu Aprili 2021, na sasa atasimamia haki miliki zote zitakazotokana na bidhaa zinazotumia nembo ya Kobe Bryant (KB24).

 

Nembo hiyo ya kibiashara (KB24) inajumuisha; Tovuti za mitandao, Kambi za michezo, Vipindi vya runinga, Filamu, Podcast pamoja na Muziki, pia nembo hiyo itajumuisha Mashati, Kadi za michezo pamoja na vyombo vya chakula na vinjwaji.

Cc; @bakarimahundu

Leave A Reply