The House of Favourite Newspapers

Mjengo wa Naira Marley Hatari!

0

 

RAPA anayekuja juu kunako muziki wa Afrika akitokea Nigeria, Azeez Adeshina Fashola ‘Naira Marley’, amedo ndosha balaa la mjengo wake wa hatari.

Naira aliposti picha kwenye ukurasa wake wa Insta akionesha mjengo wake huo mkali ulioko mjini Lake huko Nigeria ikiwa ni mjengo wake wa tano.

Naira amekuwa ni mwanamuziki ambaye amefaidika na muziki kwa muda mfupi, kwani mwaka 2019 ulikuwa ni mzuri kwake kama ilivyokuwa kwa wanamuziki wakubwa nchini humo kama Wizkid na Davido kwa kufanya shoo kali na ziara mbalimbali.

Naira alijipatia umaarufu baada ya kutoka gerezani alipokuwa akitumikia kifungo kwa kosa la kuachia Ngoma ya Am I a Yahoo Boy ambayo ni ilimpa tuhumu za kujihusisha na kundi la vijana wahalifu wa kutakatisha fedha nchini Nigeria.

STORI: HAPPYNESS MASUNGA

Leave A Reply