The House of Favourite Newspapers

Mlela Asimulia Alivyonusa Kifo

0
Yusuf Mlela

 

MWIGIZAJI wa Bongo Muvi, Yusuf Mlela amesimulia mazingira yote ya namna alivyonusa kifo, kufuatia ajali aliyoipata hivi karibuni iliyosababisha kulazwa hospitalini kwa siku kadhaa.

 

Mlela aliliambia Wikienda kuwa, alipata ajali hiyo ya gari huko Mombasa nchini Kenya, majira ya usiku alipokuwa akielekea klabu kuhudhuria shoo ya wasanii kutoka Bongo, Ben Pol na G-Nako, baada ya gari alilokuwa akitumia na rafiki zake kupoteza mwelekeo na kugonga kalavati na kuviringika mara mbili, hivyo akapoteza fahamu na kuchanika sehemu ya juu ya mdomo ambapo alipozinduka akajikuta hospitalini.

 

Mlela alisema kuwa, waliondoka nyumbani kwa mwendo wa kawaida, lakini wakiwa njiani gari lilianza kuyumba na baadaye dereva kushindwa kulidhibiti hivyo kuparamia ukingo wa kalavati hilo.

 

“Ninamshukuru sana Mungu kwa kuninusuru na roho ya kifo vinginevyo sasa stori ingekuwa tofauti kabisa, ajali isikie kwa wengine, nashangaa hata huu mdomo umeponaje na kurudia hali yake ya kawaida maana ulichanika ile mbaya,” alisema Mlela.

 

Stori: Brighton Masalu, Dar

Leave A Reply