The House of Favourite Newspapers

Mo Music Amchokonoa Barakah The Prince

0
Msanii wa Bongo Fleva, Moshi Katemi `Mo Music’

 STORI: MAYASA MARIWATA, RISASI JUMAMOSI, MKITO NUSUNUSU

MSANII wa Bongo Fleva, Moshi Katemi `Mo Music’ ameonyesha kumchokonoa mwanamuziki mwenzake, Barakah The Prince baada ya kuibuka na kusema kwa kipindi kirefu amekuwa akimzimikia mwanadada Najma ‘Naj’ ambaye ni mwandani wa msanii huyo.

Akibonga na Mikito Nusunusu, Mo Music alisema kwa jinsi anavyomkubali mrembo Naj kama yeye ndiye angekuwa anatoka naye kimapenzi angeshamuoa kitambo kwani ni msichana mzuri na mwenye sifa za kuwa mke mwema hivyo akiona Barakah anazidi kumpotezea muda atatangaza ndoa haraka iwezekanavyo.

“Kipindi najipanga kumtokea Naj ndipo Barakah akaniwahi, lakini siku zinakatika anaishia kumuuzisha sura mitandaoni wakati mimi sikutaka kumpotezea muda kabisa, isitoshe wazazi wangu wamenisihi nioe mwaka huu kama itakaribia mwisho wa mwaka bado hajamuoa, mimi nitamchumbia Naj na kumuweka ndani,” alisema Mo Music.

Leave A Reply