The House of Favourite Newspapers

Mobeto Kurudi Shule

0

MWANAMITINDO maarufu Bongo Hamisa Mobeto kwa mara ya kwanza amesema kuwa anatarajia kujiendeleza elimu ya juu mwakani.

Akipiga stori na AMANI mwanamama huyo mwenye mvuto wa aina yake alisema kwamba mara nyingi amekuwa na mawazo ya kurudi shule lakini majukumu yanamzidi hivyo anajikuta hatimizi malengo yake hayo.

“Natamani kurudi shule kujiendeleza kielimu, lakini majukumu yanakuwa mengi kiasi kwamba najikuta sitimizi hilo lengo, lakini Inshaallah Mungu akijaalia basi mwakani nitafanya hivyo,” alisema Hamisa ambaye kwa sasa ana elimu ya kidato cha nne.

 

Stori: Memorise Richard

Leave A Reply