The House of Favourite Newspapers

Gabo Hana Mipaka ya Simu na Mkewe!

0

MSANII wa Bongo Muvi, Salim Ahmed ‘Gabo’ amesema kuwa hana mipaka ya simu kwa mke wake, amempa uhuru wa kushika simu yake muda wowote anaotaka.

Akizungumza na AMANI, msanii huyo alisema kuwa mke wake ni muelewa hivyo amempa uhuru wa kushika simu yake vile anavyojisikia kwa sababu haoni sababu ya kumficha kila kitu.

“Unajua kitu ambacho wanaume wengi wanakosea ni kuwanyima uhuru wake zao, na asilimia kubwa ya wanaume wanadhani kumpa mke wako simu aitumie muda wote anaotaka ni ushamba, sio kweli kama umeamua kumuweka ndani kuna haja gani kwa wewe kumficha kila kitu? Mimi mke wangu anashika simu yangu muda wote na mimi hivyohivyo nashika yake, hakuna tatizo kabisa,” alisema Gabo.

Stori: Memorise Richard

Leave A Reply