The House of Favourite Newspapers

Mondi Aibukia India, Dude Lapikwa

0

Baada ya kubamba katika nchini mbalimbali za barani la Afrika, Mkali wa Bongofleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ sasa ameelekeza nguvu katika Bara la Asia baada ya kuonekana studio akipika ngoma mpya na staa kutoka India, Diljit Dosanjh.

 

Diamond ambaye yupo Marekani tangu aliposhiriki tuzo za BET Juni 28 mwaka huu, ameposti picha katika mtandao wake wa Instagram akiwa studio na msanii huyo na kuandika Trust me India, i got you Covered!

 

Naye Diljit Dosanjh ambaye pia ni muigizaji na mtangazaji huku akiwa na wafuasi milioni 11.2 kwenye mtandao huo, kupitia akaunti yake aliposti picha akiwa na Mondi studio kisha kuandika Nakupenda Regina Ooh! Mondi naye akajibu, World Hit yaani ngoma kali.

 

Wimbo wa mwisho aliouachia Diljit Dosanjh mwaka jana una watazamaji milioni 172.
@mushigabriel,
@hotpot_tz

Leave A Reply