The House of Favourite Newspapers

Mondi Ampagawisha Zari ‘Ndinga’ la Mil. 300

0

DARESSAL AA M: KITENDO cha staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au Mondi kumnunulia mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, gari la kisasa aina Bentley Continental GT, kimedaiwa kuzidi kumpagawisha mlimbwende huyo, RISASI linakupalia uhondo.

 

Mondi ambaye Juni mwaka huu amekuwa msanii wa kwanza katika nchi za ukanda wa Jangwa la Sahara kufikisha watazamaji bilioni moja kwenye akaunti ya YouTube, amezidi kunogesha ukaribu wake na Zari baada ya kumwagana Februari 2018.

 

Hata hivyo, zawadi hiyo ya gari yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 300, imeelezwa kuchagiza ‘ndoa’ ya wawili hao, ambao wamedaiwa kurudiana kwa siri tangu Aprili mwaka huu.

 

Kwa mara ya kwanza, Zari aliposti gari hiyo kwenye mtandao wake wa Instagram, na kuandika maneno yanayodhihirisha kuwa amepewa zawadi kutoka kwa ‘Baba T’ jina ambalo mwamama huyo wa watoto watano hupenda kumuita Mondi.

 

Hata hivyo, picha hiyo mbali na kuibua gumzo, pia wachangiaji katika mtandao huo, walipigia mstari taarifa za uwepo wa ndoa ya wawili hao ambao wana watoto wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan.

 

BENTLEY CONTINENTAL GT NI GARI GANI?

Bentley Motor Limited, inafahamika zaidi kwa jina la Bentley, ni kampuni ya kuunda magari iliyoanzishwa na raia wawili ambao ni ndugu kutoka Uingereza H. M. Bentley na Walter Owen Bentley mwaka 1919, na baadaye ikanunuliwa na Volkswagen Group mwaka 1998.

 

Bentley wamejiwekea rekodi ya kuunda magari ya kisasa na mengi yamekuwa yakitumiwa na watu maarufu wakiwemo mastaa wa muziki, filamu, michezo, viongozi wa taasisi n.k.

Aidha, Bentley Continental GT pia ni mojawapo ya brands zinazoongoza kwa kutoa misaada kwenye maeneo mbalimbali duniani.

STORI: MWANDISHI WETU, RISASI JUMAMOSI

Leave A Reply