The House of Favourite Newspapers

Mourinho, Conte Bifu Zito

Jose Mourinho

MAKOCHA Jose Mourinho wa Manchester United na Antonio Conte wa Chelsea wameendeleza bifu lao kwa kutoleana kashfa nzito.

Mourinho ndiye alianza uchokozi wiki iliyopita baada ya kudai kuwa hawezi kuwa kocha anayerukaruka kwenye benchi kila mara.

Alitoa hoja hiyo alipoulizwa baada ya mechi ya Everton siku ya mwaka mpya kuwa kwanini siku hizi amekosa uchangamfu.

Antonio Conte wa Chelsea.

“Mnataka na mimi niwe aina ya kocha anayeruka naruka ovyo kama kichaa kwenye benchi,” alijibu Mourinho.

Conte alichukulia kitendo kile kama kijembe kwake kwani yeye ndiye hupenda kuruka ruka na au kukimbilia kwa mashabiki kushangilia nao pale timu yake inapofunga.

 

“Nadhani Mourinho ana ugonjwa wa kusahau kwani hamkumbuki mambo anayofanya kwenye benchi au maneno yake ya kashfa anayoongea kila mara,” alisema Conte, ambaye alichimba mkwara kuwa hatanyamaza tena ikiwa itatokea kocha akamkashifu.

Hata hivyo, akizungumza juzi baada ya timu yake kuilaza Bristol City mabao 2-0 kwenye mechi ya Kombe la FA, Mourinho alijitetea alipozungumzia suala la kocha kuruka ruka hakuwa na maana ya Conte bali alikuwa anajizungumzia mwenyewe.

 

Mourinho alikiri kuwa ana madhambi mengi ya siku za nyuma lakini akarusha tena kijembe kingine kwa Conte.

“Mimi ni binadamu na kuna mambo mengi tu yasiyokuwa mazuri nimefanya siku za nyuma lakini kama kocha sijawahi kupata tuhuma za upangaji matokeo,” alisema Mourinho likiwa dongo kwa Conte, ambaye aliwahi kupatikana na tuhuma za mambo hayo.

 

Conte alifungiwa mwaka 2011 na Shirikisho la Soka la Italia kwa kosa la kushindwa kuripoti masuala ya upangaji matokeo wakati akiwa Kocha wa Sienna.

Aliadhibiwa kutokaa kwenye benchi mechi 10 lakini alitumikia mechi nne kabla ya kufutiwa tuhuma hizo ambazo Mourinho alitonesha kidonda jana.

 

Mourinho na Conte kwa muda mrefu wamekuwa na bifu lililoanzia wakati wakifundisha soka nchini Italia. Mourinho alikuwa Inter Milan na Conte akiwa Juventus.

 

Bifu hilo limeendelea England ambapo Mourinho amewahi kumshutumu Conte kwa kuzikosea adabu timu pinzani kwa ushangiliaji wa kupitiliza timu yake inaposhinda na pia kuna mechi hawakushikana mikono ikiwa ni mwendelezo wa uadui baina yao.

Live: ACT Wazalendo Kufanya Kazi Na Ukawa Mwaka Huu

Comments are closed.