MWANDISHI WETU | CHAMPIONI, Dar es Salaam
WAKATI mamia ya wasomaji wa magazeti ya Global Publishers wakiendelea kujaza kuponi kwa ajili ya shindano la awamu ya pili ya Shinda Nyumba, leo Jumatatu Mr Championi atakuwa mitaani jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kugawa zawadi kwa wasomaji hao.
Ofisa Masoko wa Global Publishers, Jimmy Haroub akimuelekeza msomaji namna ya kujaza kuponi ya Shinda Nyumba.
Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, Mr Championi atampatia zawadi msomaji yeyote atakayekutwa akijaza kuponi hiyo mahali popote.
“Hii ni sapraizi kwa wasomaji wetu, Mr Championi atakuwa akikatiza katika mitaa mbalimbali jijini Dar na kumsapraizi yeyote atakayekutwa akijaza kuponi yake tayari kuituma kwetu, hatuwezi kusema tutatoa kitu gani, lakini ni kitu ambacho kitamfurahisha msomaji,” alisema Mrisho.
Mr. Uwazi akigawa zawadi ya kofia kwa msomaji ba mkazi wa Goba.
Alitumia nafasi hiyo kuwataka wasomaji kujiweka tayari kupokea zawadi yao mara tu wakimuona Bwana Championi mitaani na kuwa wasisahau kujaza kuponi zao mara baada ya kununua magazeti hayo ambayo ni Championi, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.
Droo ya kwanza ndogo kwa ajili ya shindano hilo itachezeshwa Februari 8, mwaka huu na baada ya hapo, kila mwezi itafanyika droo nyingine ambapo zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi.
Katika tukio hilo la kwanza, zawadi zitakazotolewa ni pamoja na pikipiki, televisheni, simu aina ya smartphones na vyombo vya ndani.
Global Publishers juzi iliwafikia wasomaji wake wa maeneo ya Msasani, Tandale, Magomeni, Mwananyamala, Sinza na kwingineko ambapo wamejitokeza kwa wingi kununua magazeti na kujaza kuponi kwa ajili ya kushinda nyumba awamu ya pili.
Msomaji akizawadiwa tisheti baada ya kununua gazeti la Uwazi.
“Nawakubali sana Global na mimi nimeamua kushiriki baada ya kugundua kuwa Shinda Nyumba ni ya ukweli baada ya kumuona mshindi kutoka mkoani Iringa akizungumza mwenyewe kuwa kashinda kwa kununua magazeti yenu,” alisema Yusuph wa Tandale.
Wakazi wa Goba ambao pia walitembelewa na timu ya Shinda Nyumba, nao walisema hawawezi kukaa kimya bila kupata kuponi za shindano hilo wakati kila mmoja hivi sasa anazungumzia kuhusu zawadi bwerere kutoka Global Publishers.
“Siyo lazima mtu ushinde nyumba maana hiyo ni zali la mentali kweli, lakini jamani hivi vitu kama simu na vyombo vya nyumbani uvikose? Mimi natamani sana simu ya tachi, nitajaza kuponi hadi nipate,” alisema Consolata Simon, aliyekutwa kijiweni kwake kwa mama ntilie, huko Goba.
Msomaji mwingine Unaris Yunus, wa Goba njia panda, alisema awamu ya kwanza ya Shinda Nyumba hakuweza kupata zawadi yoyote, lakini safari hii moyo wake unamsukuma kuamini atakuwa miongoni mwa washindi.
Msomaji akizawadiwa tisheti ya Shinda Nyumba
“Kwanza nasikia zawadi zimeongezeka, sasa kama mnavyosema pikipiki itatolewa kila mwezi, sasa nikose nyumba sawa, basi pikipiki, televisheni, simu, mashuka, branketi hadi vyombo vya ndani nikose? Aaah jamani, Mungu nisaidie,” alisema Yunus.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho alizidi kuwasisitiza wasomaji kuhakikisha wanajipatia kuponi za kutosha tayari kwa droo ndogo ya kwanza ambayo itafanyika hiyo Februari 8, mwaka huu.
Msomaji akijaza kuponi ya Shinda Nyumba.
“Utaratibu wetu wa kutuma kuponi ni uleule, baada ya kununua gazeti letu lolote kati ya Championi, Risasi, Uwazi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda, kata kuponi kisha jaza kwa kadiri ilivyoelekezwa, halafu peleka kwa wakala yeyote aliye jirani na wewe, maana mawakala wetu wapo nchi nzima, au kwa wale wa Dar es Salaam, wanaweza kuzileta katika ofisi zetu zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar,” alisema.
Kwa stori zote kali, Tucheki…
Facebook @Globalpublishers
Twitter @GlobalHabari
Instagram @GlobalPublishers
YouTube @GlobalTVTZ
Endelea kutembelea website ya Global Publishers kila siku, tutaendelea kukusogezea kila news inayotokea mahali popote duniani.
Comments are closed.