The House of Favourite Newspapers

Mr Eazi Aachia Ngoma Mpya ya ‘The Don’

0

MSANII mahiri wa Afro Pop, Mr Eazi ameachia video ya wimbo wake mpya, The Don, ambao ni wa kwanza katika EP (Extended Play) yake ya Something Else.

 

Video hiyo iliyojaa ubunifu mkubwa, imeongozwa na mtayarishaji maarufu wa filamu, Babs Direction na imerekodiwa nchini Ghana ambapo ndani yake, kuna kisa cha The Don, mhalifu ambaye ametoroka jela na kuendelea na maisha yake ya mtaani na familia yake.

 

Mr Eazi anaeleza kwamba ilibidi atumie akili nyingi kuandika wimbo huo kwa sababu kwa mwaka mzima wa 2020 alikua bize kutengeneza platform yake ya emPawa Africa.

 

Anaelekeza shukrani zake kwa maprodyuza wa wimbo huu, Kel P na Killertunes kwa moyo waliouonesha kwani walikua wakimfuata jijini Accra mpaka alipofanikiwa kurekodi wimbo huo.

 

Kwa Eazi, Albamu ya Something Else ni mwendelezo wa safari yake ya kimuziki, ikiwa ni albumu ya nne baada ya kutoa album tatu za awali ambazo ni Life is Eazi, Vol. 1 Accra to Lagos ya mwaka 2017, Life is Eazi, Vol 2 Lagos to London ya mwaka 2018 kabla ya kupata maarufu mkubwa duniani kote.

 

Mr Eazi kwa sasa yupo nchini Ghana akiendelea na kazi aliyoianza ya kuandaa albamu yake ya tatu inayokwenda kwa jina la Life is Eazi Vol 3 ambayo itafuatana na EP hiyo ya Something Else.

 

Albamu hiyo itakuwa ikipatikana kwenye majukwaa ya DSP na emPawa Africa inayomilikiwa na Mr Eazi chini ya lebo yake, Banku Music.

 

Na Mwandishi Wetu

 

Tazama “The Don” YouTube:

Leave A Reply