The House of Favourite Newspapers

KUTOKA MOSHI: IBADA YA MAZISHI YA MZEE MENGI – VIDEO

MWILI  wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi,  umewasili katika kanisa la  (KKKT – Usharika wa Moshi Mjini) kwa ajili ya ibada na kuagwa kabla ya maziko yatakayofanya baadaye leo Alhamisi, Mei 9, 2019, nyumbani kwao Machame, Kilimanjaro.

Ibada ikiendelea kanisani. 

Mamia ya waombolezaji wakiwemo viongozi wa serikali, vyama vya siasa, wabunge, viongozi wa dini na wananchi wamefika kanisani hapo kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho.

Wasanii mbalimbali wakiwa katika ibada hiyo.

Madame Ritta  na Balozi wa Ghana nchini China, Edward Boateng, aliyekuwa swahiba wa marehemu Mengi, wakiwa kanisani.

 

 

Jeneza la mwili wa Dr. Mengi likishushwa ili kupelekwa kwenye ibada.

Balozi wa Ghana nchini China, Edward Boateng ndiye mtu ambaye marehemu Mengi alimfuata mwaka 1993 na kumuomba ampe njia za kuweza kufungua kituo cha televisheni chini hapa. Hii ni kutokana na kwamba Boateng alikuwa mzoefu katika jambo hilo kwani alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni inayomiliki vituo vikubwa vya televisheni duniani kama CNN na Cartoon Network.

 

 

Boateng amesema alimwezesha Dkt. Mengi  kuanzisha kituo binafsi cha kwanza cha televisheni nchini, na kwamba alikuwa na mpango wa kwenda kuzindua kitabu chake cha ‘I can, I will, I must’ nchini Ghana.

 

Baadhi ya waombelezaji wakifuatilia tukio hili la kuagwa kwa mwili wa mpendwa wetu Dkt. Mengi nje ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Usharika wa Moshi Mjini.

 

Baadhi ya waombelezaji wakifuatilia tukio la kuagwa kwa mwili wa Mengi.

Familia ya marehemu Mengi ikiingia kanisani. 

Waombolezaji wakiwa nje ya kanisa.

 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (kulia) akiwa na mwanaye wa kwanza.

 

Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Nnauye (kushoto), Anne Kilango Malecela (CCM)  na Joseph Mbatia (NCCR-Mageuzi) wakiwa kanisani.

FUATILIA TUKIO LOTE HAPA

Comments are closed.