The House of Favourite Newspapers

Mtoto Amnyima Usingizi Jux

0

 

DAR: Staa wa miondoko ya RnB Bongo, Juma Mussa ‘Jux’ ameeleza namna ambavyo ishu ya kupata mtoto inavyomkosesha usingizi hivyo anatamani kupata mtoto wa kike.

 

Jux amesema sababu za kutaka mtoto wa kike ni kwamba anaamini kwenye kuwekeza kwa mwanamke kwa sababu atakuwa na uwezo wa kusaidia wengine.

 

“Nimesema mtoto wangu wa kike wa kwanza, ila anaweza akawa hata wa pili kama nikipata wa kiume wa kwanza ila awe mtoto wa kike, nitamlea katika akili ili aweze kujitegemea zaidi, naamini kwenye kuwekeza kwa mwanamke ili ajitegemee kwa sababu kuna vitu vingi sana vitakuwa vizuri na ataweza kusaidia watu wengi sana,” amesema Jux na kuongeza;

 

“Mwanamke ambaye anaweza kujitegemea atakuwa vizuri kwenye maisha kuliko anayemtegemea mtu, kwa hiyo mimi hicho ndiyo kitu ambacho ninakiangaliaga sana, hata kwa mtu ambaye nakuwa naye kwenye uhusiano huwa ninamuangalia kama ana uwezo wa kujitegemea na hata kama hawezi nitamtengenezea mazingira aweze kujitegemea bila mimi.”

Stori: NEEMA ADRIAN, Ijumaa

Leave A Reply