The House of Favourite Newspapers

Museveni Amteua Mtoto wake Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa Mkuu mpya wa Majeshi (CDF)

0
Jenerali Muhoozi Kainerugaba

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amemteua Mtoto wake Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa Mkuu mpya wa Majeshi (CDF) Nchini Uganda akichukua nafasi ya Jenerali Wilson Mbasu Mbadi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri anayehusika na masuala ya biashara kwenye mabadiliko mapya aliyofanya katika Baraza la Mawaziri la Nchi hiyo usiku huu.

Muhoozi aliwahi kuwa kwenye nafasi ya Ukamanda wa Jeshi la Ardhini la Uganda kabla ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo mnamo Oktoba 04, 2022 huku nafasi yake ikichukuliwa na Meja Jenerali Kayanja Muhanga ambaye alikuwa Kamanda wa Operesheni Shujaa inayoendeshwa Nchini DRC.

RAIS SAMIA AIONA VIDEO ya GLOBAL TV ya MTOTO RAMA ANAYEUMWA FIGO – “AKATIBIWE BURE MUHIMBILI”…

Leave A Reply