The House of Favourite Newspapers

Mwakinyo: Kuna Watu Wananichukia – Video

0

BONDIA namba moja Tanzania na Afrika, Hassan Mwakinyo amesema wapo baadhi ya Watanzania wanaomchukia kutokana na mafanikio anayoyapata kupitia tasnia ya mchezo wa ngumi ambapo kwa sasa ndiye anayeibeba Tanzania.

 

Akizungumza baada ya mechi yake na Bondia wa Namibia, Julius Munyelele Indongo, huku akimshuruku mama yake mzazi kwa sapoti anayompa, Mwakinyo amesema hawezi kukata tamaa, anachokiangalia ni kufanya vizuri kila siku, hata wanaomkataa ipo siku watamkubali.

 

Aidha, Mwakinyo amesema bondia aliyempiga (Indongo), siyo bondia mdogo ni bondia mkubwa Afrika mwenye heshima kubwa na anashikilia mataji makubwa hivyo wasimbeze hata kidogo kwani amepambana vya kutosha mpaka kufanikiwa kumchapa.

 

Mwakinyo amefanikiwa kutetea ubingwa wa Super Welterweight baada ya kumpiga Indongo maarufu kama Blue Machine katika Raundi ya nne tu ya mchezo kwa TKO kwenye pambano lilofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Ubungo Plaza.

 

Leave A Reply