The House of Favourite Newspapers

Mwanajeshi Akamatwa kwa Kuvalishwa Pete Akiwa na Sare za Jeshi

0

MWANAJESHI wa kike amekamatwa nchini Nigeria kwa kukubali ombi la kuolewa akiwa amevalia magwanda rasmi ya kijeshi jambo ambalo limetajwa kuwa ni kinyume cha taratibu za nidhamu ya kijeshi.

 

Ofisa huyo anatuhumiwa kukiuka kanuni za maadili za kijeshi kwa kujiingiza katika mapenzi akiwa amevalia sare za Jeshi la Nigeria, pia ni kinyume na sera za Jeshi kuhusu masuala ya matumizi ya mitandao ya kijamii.

 

“Kazi ya wakufunzi ilikuwa kuwafunza kikosi cha vijana na kutojiingiza katika uhusiano wa kimahaba na yeyote kati yao,” Msemaji wa Jeshi hilo, Jenerali Clement Nwachukwu.

 

Video iliyosambaa mitandaoni wiki iliyopita ya askari huyo akivalishwa pete kutoka kwa mwanamume aliyepiga magoti mbele yake, huku watazamaji wakishiriki furaha ya wapenzi hao. Kundi la kutetea haki za wanawake limeshutumu jeshi kwa kumbagua.

Wanadai kuwa hatua kama hiyo haikuwa imechukuliwa dhidi ya wanajeshi wa kiume waliohusika katika maonyesho ya hadharani ya mahusiano ya kimahaba wakiwa wamevalia sare kamili za kijeshi,” Kikundi cha Women Empowerment and Legal Aid.

 

Mwanaharakati wa haki za binadamu na aliyekuwa mgombea urais wa Nigeria Omoyele Sowore alilaani uamuzi wa jeshi na kuuita “udhalilishaji”.

 

Mwanajeshi huyo alikuwa amekubali pendekezo la ndoa kutoka kwa mwanafunzi katika mpango wa mafunzo kwa vijana wa serikali, anayejulikana kama Kikosi cha Huduma ya Vijana kwa Kitaifa (NYSC). Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii waliwapongeza wanandoa hao, na kumsifu mwanamume huyo kwa kupendekeza. Wengine walimtania askari huyo.

Leave A Reply