The House of Favourite Newspapers

Tshala Muana Mbaroni Akidaiwa ‘Kumnanga’ Rais

0

SHIRIKA la kutetea haki za binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (ACAJ), linataka maofisa wa usalama nchini humo kumwachilia huru mwanamziki maarufu Tshala Muana ambaye alikamatwa Jumatatu mjini Kinshasa.

 

Polisi walimkamata mwanamziku huyo mweye umri wa miaka 62 baada ya kutoa wimbo ambao wachambuzi nchini humo wanasema kwamba tafsiri yake inamdhalilisha rais wa sasa nchi hiyo, Felix Tshisekedi, japo wimbo huo hautaji mtu yeyote.

 

Ujumbe katika wimbo huo uitwao ‘Ingratitude’ unamlenga mtu ambaye amepewa kila analotaka maishani lakini amekosa kufanya mema wakati yupo madarakani. Mwanamziki huyo ana uhusiano wa karibu na familia ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Joseph Kabila. Kulingana na mwandishi wetu aiyeko nchini humo, Austere Malivika, Tshala Muana amekamatwa na polisi ili kutoa maelezo zaidi kuhusu wimbo wake.

 

Wimbo huo umetolewa wakati kuna mvutano kati ya Rais Tshisekedi na viongozi wa vyama vinavyomuunga mkono ambavyo vinaongozwa na watu walio karibu na rais mstaafu, Joseph Kabila.

 

Wakati huohuo, maandamano yameripotiwa kufanyika mjini Kinshasa baada ya kuenea habari kwamba Tshala Muana amekamatwa.

 

Imetayarishwa na Kennes Bwire,VOA, Washington DC.

 

Leave A Reply