The House of Favourite Newspapers

MWILI WA MAMA WA SHIGONGO WAWASILI NYUMBANI MIKOCHENI – VIDEO

Gari lenye mwili wa marehemu Asteria Kapela likiwasili nyumbani Mikocheni B, jijini Dar es Salaam jioni ya leo.

MWILI wa Mama Mzazi wa Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, Bi. Asteria Kahabi Kapela umewasili nyumbani kwake maeneo ya Mikocheni B, jijini Dar es Salaam leo saa 10:00 jioni kwa ajili ya shughuli ya kuagwa itakayofanyika kesho Jumapili.

Mtoto wa Marehemu, Eric Shigongo (aliyeshika kiuno) akiwa na Mbunge Mwigulu (kushoto) na waombolezaji wengine wakijiandaa kuupokea mwili wa marehemu baada ya kuwasili nyumbani.

Bi. Asteria Kahabi Kapela alifariki dunia alfajiri ya jana Ijumaa, Julai 27, 2018 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akitibiwa baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mtoto wa marehemu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Global Publishers, Lydia James Bukumbi akilia kwa uchungu kuondokewa na mama yake.
Watoto wa marehemu wakisaidiwa kuingizwa ndani.

Mwili ukishushwa kwenye gari.

 

 

Mwili ukiingizwa ndani.
Shigongo akiliinamia jeneza lenye mwili wa mama yake.

 

Shigongo akilia kwauchungu.
Mjukuu wa Marehemu, Asteria Aaron akilia kumpoteza bibi yake.

 

 

Mkwe wa marehemu ambaye ni mke wa Shigongo, Veneranda Ephraim akilia kwa uchungu kumpoteza mama.

BREAKING: Mwili wa Mama Shigongo Ukiwasili Nyumbani Muda Huu

PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL

Comments are closed.