The House of Favourite Newspapers

Mzee Magali Asimulia Mateso ya Corona Marekani

0


DAR: Msanii wa filamu za Kibongo ambaye kwa sasa anafanyia shughuli zake Chicago nchini Marekani, Charles Magali ‘Mzee Magali’ amesimulia kuishi kwenye mateso kutokana na virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 ambavyo vimeua zaidi ya watu 5,000 nchini humo.

Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa njia ya simu, Mzee Magali alisema kwa sasa wamekuwa wakiishi kwa kuomba Mungu huku wakizingatia masharti ya wataalamu wa afya kila yanapotolewa.
“Huku ugonjwa wa Corona ndiyo tishio kubwa, kwa sasa watu wengi tumekuwa tukijifungia ndani hali inayosababisha dili nyingi kusitishwa.

“Unajua kitu ambacho hakikuwahi kutokea, kukizoea ni vigumu sana maana tumeshazoea kuwa huru na kufanya kazi kwa kujiachia, lakini kwa sasa inashindikana kabisa.

“Yaani hili ni balaa, tumuombe Mungu lipite, maana inapofikia mtu unashindwa kwenda kwenye shughuli zako za uzalishaji, hiyo ni hatari maana unaweza kufa kwa njaa,” alisema Mzee Magali ambaye ni tishio kwa filamu za kibabe hapa nchini.

Kwa miaka kadhaa, sasa mkongwe huyo wa filamu anaishi nchini humo na aliwahi kusema anawatengenezea mazingira wasanii wa Kibongo wakafanye kazi huko ambako amedai kazi hiyo inalipa zaidi kama utajituma.

STORI: RICHARD BUKOS, RISASI JUMAMOSI

Leave A Reply