The House of Favourite Newspapers

Mzimu wa Masogange wamtesa Rammy

0

MWIGIZAJI Rammy Galis amesema bado mzimu wa aliyekuwa video vixen maarufu Bongo, marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’ unamtesa.

 

Rammy amelieleza Risasi Jumamosi jinsi anavyotokewa na Masogange kwenye mazingira tofauti.

 

“Yaani imekuwa ni ngumu sana kumsahau Masogange, kuna wakati siamini kama amekufa, lakini kuna wakati nasikia kama ananiita au namfananisha na mtu njiani au naweza nikaingalia filamu yetu tuliochezaga pamoja hata kwa wiki mara mbili,” alisema Rammy ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Masogange aliyefariki dunia mwaka jana.

Stori: Imelda Mtema

 

Leave A Reply