The House of Favourite Newspapers

Nabii Aliyetabiri Ajali ya Ndege Iliyoua Watu 19 Bukoba, Adai Alioneshwa Kiroho.. -Video

0

Taifa la Tanzania linaomboleza vifo vya watu 19 huku wengine 24 wakiokolewa hai kufuatia ajali mbaya ya ndege ya Shirika la Precision Air iliyotokea juzi Jumapili, Novemba 6, 2022 katika Ziwa Victoria baada ya kushindwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba kutokana na hali ya hewa.

 

Mtumishi wa Mungu, Pastor Malachi amewashangaza wengi baada ya video yake kusambaa ikimwonyesha akitoa unabii juu ya ajali hiyo ya ndege takribani wiki zilizopita kabla ya ajali kutokea.

 

Mchungaji huyo wa Kanisa la Christ Mandate alitoa unabii huo kwenye ibaada maalum na maombi Oktoba 20, 2022, katika Kanisa hilo lililopo Kigogo, jijini Dar es Salaam mkabala na Kituo cha Polisi Kigogo na kusema; Baada ya kutoa unabii huo, Pastor Malachi ambaye amekuwa maarufu kwa kutoa mapepo, kuharibu nguvu za giza zilizokufunga, magonjwa sugu kama kisukari na presha, aliwaongoza waumini wote katika kuliombea tifa na kulikabidhi mikononi mwa Mungu ili kuepukana na mauti ambayo yangesababishwa na ajali hiyo.

 

⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply