The House of Favourite Newspapers

Nafasi za kazi 30 Madereva wa Magari makubwa – PRIMEFUELS Tanzania Ltd

0

PRIMEFUELS TANZANIA Limited ni Kampuni inayohusika na Usafirishaji wa Mizigo tofauti yenye asili ya vimiminika (fluids) na mali yabisi (dry cargo).

PRIMEFUELS TANZANIA Limited inahitaji madereva wenye WELEDI, UZOEFU NA UADILIFU wa hali ya juu usiotiliwa shaka na mtu au taasisi yoyote ndani na nje ya nchi.

Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa na vigezo vifuavyo wakizingatia vigezo vikuu vitatu vilivyotajwa hapo juu;

  • Umri usiopungua miaka 25 na usiozidi miaka 45.
  • Elimu ya kidato cha nne na kuendelea.
  • Afya inayostahimili safari za nje na ndani ya nchi.
  • Uwezo wa kusoma na kuandika lugha ya Kiingereza na Kiswahili fasaha.
  • Uzoefu wa kuendesha magari makubwa usiopungua miaka mitano.
  • Ujuzi na uzoefu wa kuendesha gari za kusafirisha mafuta (Tankers)
  • Leseni ya Udereva yenye sifa ya kuendesha magari makubwa
  • Nyaraka za kusafiria (Passport)
  • Picha 3 za rangi (Passport size Photos)
  • Barua za wadhamini wawili zenye picha zao na anuani ya makazi
  • Barua ya serikali ya Mtaa unamoishi ikiwa na namba ya simu ya kiongozi wa serikali ya mtaa aliyekupa barua hiyo.

MAOMBI YOTE YALETWE OFISINI KWETU KUANZIA TAREHE 15-10-2019 KWA NJIA YA MKONO NA KUKABIDHIWA KWA WALINZI WETU, NA KUJAZA KWENYE KITABU MAALUMU. OFISI ZETU ZIPO KIPAWA, KIWANJA NAMBA 139, NYERERE ROAD, MKABALA NA UWANJA WA NDEGE. MAOMBI YOTE YAELEKEZWE KWA

MENEJA – RASILIMALI WATU
PRIMEFUELS TANZANIA LIMITED
S. L. P. 2873, DAR ES SALAAM

MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 25-10-2019

Zingatia – Muhimu:

  1. Watakaochaguliwa watapigiwa simu na ofisi kwa mchakato zaidi
  2. Epuka kutapeliwa fedha au kitu chochote cha thamani kwa ahadi ya kupata upendeleo wa ajira ndani ya Primefuels.

AU

>>> KUTUMA MAOMBI BONYEZA HAPA <<<

Leave A Reply