The House of Favourite Newspapers

Naibu Waziri Dugange: Idadi Majeruhi wa Mafuriko Hanang Wanaoendelea na Matibabu Yapungua

0

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Festo Dugange amesema idadi majeruhi wa mafuriko ya tope Hanang mkoani Manyara wanaoendelea na matibabu imepungua kutoka 117 hadi 36 na sh.milioni 560 zimetolewa kwaajili ya huduma za afya kwa wathirika hao.

Dkt. Dugange akiwa ameambatana Jenista Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu na mhandisi Godfrey Kasekenya Naibu Waziri wa Ujenzi katika ukaguzi wa maeneo yaliyoathirika ambayo serikali inayarejesha kwenye hali yake katika Mji wa Katesh wilaya ya Hanang, amesema;

“Tunauhakika hao 36 waliobahi wataendelea kuruhusiwa kurejea nyumbani kuendelea na majukumu yao na jambo la muhimu kwenye majanga haya serikali inajitahidi kudhibiti magonjwa ya mlipuko kujitokeza na sehemu kama hii tulichokifanya tumeimasha mfumo ya udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwenye jamii yetu na katika kambi zetu” Dkt. Dugange

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amesema serikali imeanza mazungumzo na taasisi za kifedha ili kutoa unafuu kwa wafanyabiashara walioathiriwa na mafuriko na ameendelea kushukru wadau wanaoendelea kutoa msaada.

Waziri Jenista Mhagama amesema kuwa mbali na Serikali kurejesha miundombinu pia imeendelea kuwa bega kwa bega na Wananchi sambamba na kutoa maagizo kwa Wataalamu wa Satellite kuanza kuangalia Kaya zote na kuona zipi zimeathirika zaidi huku ikiendelea kutoa msaada zaidi.

CHID BENZ AMILILA DIRECTOR NISHER -“MMENISHTUA SINA TAARIFA YOYOTE, MUZIKI WETU UNAMSUJUDIA JAMAA”..

Leave A Reply