The House of Favourite Newspapers

Nana Gum: Najisikia Huru Kula Kwa Mama Lishe

0
Mwanamuziki anayekuja vizuri kwenye tasnia ya Bongo Fleva, Nawal Mahamoud ‘Nana Gum’ akijiandalia msosi.

 

MAMBO vipi mpenzi msomaji wangu wa Mpaka Home, kama ilivyo kawaida ya safu hii ni kutinga majumbani kwa mastaa mbalimbali na kuyaibua maisha yao halisi ya kila siku.

 

Wiki hii tumemtembelea mwanamuziki anayekuja vizuri kwenye tasnia ya Bongo Fleva, Nawal Mahamoud ‘Nana Gum’ ambaye anatamba na wimbo wake wa Tamutamu, anayeishi Kariakoo jijini Dar. Mwanamuziki huyu kafunguka vitu mbalimbali anavyopenda kufanya nje ya kazi yake ya muziki.

 

MPAKA HOME: Ukiamka asubuhi unapenda kufanya nini cha kwanza?

NANA GUM: Kiukweli nachukia sana mwili mkubwa hivyo nikiamka cha kwanza napenda kufanya mazoezi kidogo alafu nafanya usafi wa mwili wangu na kuanza kutengeneza vitafunwa mwenyewe maana sipendi vya kununua”

 

MPAKA HOME: Vipi unaweza shughuli za jikoni?

NANA GUM: Kiukweli sijisifii kabisa lakini kuhusiana na ishu ya jikoni niko vizuri sana, napika kila kitu ambacho mwanamke anatakiwa kupika na siyo mvivu jikoni kabisa

Nana akiwa jikoni na mmoja wa wanafamilia yake.

MPAKA HOME: Una mume, watoto au mchumba?

NANA GUM: Kwa sasa bado sijabarikiwa mtoto lakini nipo kwenye uhusiano na mtu ambaye sipendi kumuweka wazi.

MPAKA HOME: Ukichukia cha kwanza unafanya nini?

NANA GUM: Kwanza sipendi kuchukia hata kidogo lakini kama kitu kimenikwaza sana nitaenda kufungulia muziki mkubwa na kusikiliza kisha nitakuwa sawa tu au naondoka kabisa eneo la tukio.

…Akipiga stori na ndugu zake.

MPAKA HOME: Umeshawahi kula chakula kwa mama lishe?

NANA GUM: Tangu zamani nilisema nikiwa maarufu sitaki kujikweza kabisa hakuna chakula nachopenda kama cha mama lishe, nakuwa huru na ninapenda sana maisha hayo.

MPAKA HOME: Nyumba unayoishi ni ya nani?

 

NANA GUM: Hapa ninapoishi ni nyumbani kwetu na siwezi kutoka hapa nyumbani kwetu mpaka niolewe.

MPAKA HOME: Namba ya nani ni muhimu kwenye simu yako?

…Akiweka sawa vifaa vya jikoni.

NANA GUM: Kwa kweli namba muhimu kwenye simu ni ya mama yangu maana nikiwa na shida yoyote muhimu wa kwanza kumpigia ni yeye.

MPAKA HOME: Kitu gani hupendi kukifanya ukiwa nyumbani?

 

NANA GUM: Sipendi kabisa kuosha vyombo na kufua nguo nafanyaga tu kwa sababu mimi ndiye mwanamke peke yangu.

…Akimwagilia maua yanayopamba nyumba yao.

MPAKA HOME: Nini kero yako kubwa?

NANA GUM: Sipendi mtu kunichukulia kama kikatuni kwa sababu hata kama nina jina napenda mtu anichukulie kawaida tu kama mtu mwingine na si vinginevyo.

MPAKA HOME: Unapendelea kula chakula gani?

 

NANA GUM: Napenda sana ndizi nyama pia napenda kuzipika mwenyewe.

MPAKA HOME: Unatarajia nini katika maisha yako baada ya miaka mitano baadaye?

NANA GUM: Napenda kuja kuwa mwanamke mwenye maendeleo makubwa sana yaani niwe na kitu changu kingine nafanya nje ya muziki wangu.

MPAKA HOME: IMELDA MTEMA | RISASI JUMAMOSI – GLOBAL PUBLISHERS

KIFO CHA KANUMBA: Kioja cha Lulu Leo Mahakamani!!

Leave A Reply