The House of Favourite Newspapers

Nandy, Rayvanny Kitanuka Muda Wowote!

0

Dar: Sexy lady wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ na mkali mwezake, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, wako tayari kukinukisha muda wowote.

 

Nandy na Rayvanny, kila mmoja ameeleza ujio wa projekti yao mpya muda wowote kuanzia sana. Kwa mujibu wa Rayvanny, ngoma mpya ipo mbioni hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula muda wowote kuanzia sasa.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny amewaomba mashabiki wake wamsaidie kuamukia ni lini aachie projekti yake mpya.

 

Hatua hiyo na Rayvanny inakuja baada ya mmoja wa mameneja wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) anayoitumikia, Sallam SK kusema kuwa, lebo hiyo ipo tayari kuachia projekti mpya zipatazo tatu ndani ya mwezi huu wa Agosti.

 

Kwa mujibu wa Sallam, moja ya projekti hizo ipo ya Diamond na nyingine ni ya Rayvanny. Kwa upande mwingine, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nandy naye aliwaomba mashabiki wake wamsaidie kuamua tarehe ya Stori: Happyness Masunga Ijumaa kuachia ngoma mpya.

 

Kwa sasa, Nandy anakimbiza na ngoma yake ya Acha Lizame ambayo ameshirikiana na mkali anayemiliki Lebo ya Konde Gang Music Worldwide, Harmonize.

 

Projekti hiyo mpya inaaminika inawezekana Nandy ameshirikiana na msanii kutoka Kenya, Tanasha Donna kwa sababu hivi karibuni walitangaza kuwa kwenye projekti ya pamoja.

Stori: Happyness Masunga Ijumaa

Leave A Reply