The House of Favourite Newspapers

Nay, Madee Hizo Kiki Veepe?

madee1ANDREW CARLOS | IJUMAA

NAJARIBU kuyakumbuka maneno ya mwanasaikolojia, William James ambaye aliwahi kusema kuwa, hitaji la kwanza la mwanadamu ni kuthaminiwa kwa kile unachokifanya. Ukifanya kitu kizuri kwanza kitapendwa na pili kitathaminiwa. Na ukifanya kitu kibaya kwa kusudio f’lan huenda kikapendwa lakini kikakosa kuthaminiwa. Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego ni mmoja wa wakali wa Muziki wa Bongo Fleva anayefanya poa, vivyo hivyo kwa Hamad Ally ‘Madee’.

Wote wawili wamekulia Manzese jijini Dar lakini kwa muda mrefu wamekuwa katika ushindani wa kimuziki huku ubishani ukiwa ni nani rais wa Manzese japo awali Madee alikuwa akijiita hivyo. Hakuna anayetaka kujishusha mbele ya mwenzake japokuwa mwaka 2013 katika Tamasha la Fiesta mkoani Tanga, walipatana na kupeana hadi lifti kwa kupanda gari moja ya Madee.

nay-wa-mitego-14Nay wa Mitego

Mashabiki wakiwa katika kuamini kuwa wamemalizana, Nay akaibuka na Wimbo wa Salamu Zao ambapo katika ngoma hiyo kuna mistari inayoonesha wazi kutafuta kiki kwa kumponda Madee ambayo ni; “Me ndo Rais wa Manzese yule tozi kasanda, Manzese mikono juu naiongoza kamanda.”

Baada ya hapo iliendelea chinichini lakini mwaka huu wameufungua upya kwa bifu lao ambalo ni wazi linaonesha kuziweka nyimbo zao kwenye mstari (kiki). Ikumbukwe kuwa, Madee ameachia Wimbo wa Hela na Nay ameachia Sijiwezi na kila mmoja anataka ngoma yake iwe juu.

Katika Wimbo wa Hela, Madee amerudisha madongo ya Wimbo wa Salam Zao wa Nay kwa kuimba; “Yule kijana wa home siyo staa, anatukana hata waliomzaa, wivu tamaa na njaa ukiendekeza ujue kidole utakaa.” Kuonesha kuwa ilikuwa dongo kwa Nay, baada ya muda mfupi tangu wimbo huo utoke, aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram; “Leo nimesikia wimbo mbayaaaaa kuliko nyimbo mbaya nilizowahi kusikia mwaka huu. Mtag huyo msanii mwenye huo wimbo kama ushausikia..!”

madeee2Madee

Baada ya kauli hiyo, redio moja maarufu Bongo ilimtafuta Madee na kumuwekea ngoma hiyo na baada ya kuisikia alisema; “Nimeusikiliza, nimemuona Raymond (Rayvanny wa WCB) anatakiwa kurudi sehemu (Tip Top) kuwasaidia kaka zake.” TV moja ikamtafuta tena Madee na kumuonesha video ya ngoma mpya ya Nay, Sijiwezi na alipoiona alisema; “Ndo nani aliyeimba?

Halafu wimbo mbaya. Ujue nilikuwa Ulaya kwa hiyo sijaona video nyingi.” Alipobanwa kuwa mara ya mwisho kusikiliza nyimbo za Nay ilikuwa mwaka gani alisema; “Zamani sana, wimbo wake wa mwisho kusikiliza ni ule alioimba na Diamond (Muziki Gani) tena ile ilikuwa idea yangu kutoka ule wimbo nilioimba na Godzilla (Game Inavyochange).”

nay

USHAURI

Muziki wa Bongo Fleva umekuwa na umeweza kuvuka hadi boda na kujulikana Afrika. Bifu hizi ni wazi zinaonesha kiki ya kupandisha nyimbo zao lakini hazikuzi muziki wetu. Mashabiki ndiyo waamuzi wa mwisho wa nyimbo na si kulazimisha. Mwisho  wote wawili wanapaswa kuuthamini muziki kwani ndiyo uliowafikisha walipo.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.