The House of Favourite Newspapers

Nay wa Mitego: Wananchi Wangenipa Tuzo

0

RAPA maarufu Bongo anayetamba na ngoma yake mpya ya ‘Hunijui‘ ambayo ameiachia siku kadhaa zilizopita, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amesema kutokana na ukubwa wa muziki wake anaoufanya, kungekuwa na Tuzo za Muziki basi wananchi wangempa tuzo za kutosha.

“Mwaka 2021 kwangu mimi, muziki wa Rap Umekuwa mkubwa zaidi kuliko wa kuimba, ukiangalia mimi ndio msanii wa rap ambaye nimepeleka nyimbo tatu mfululizo namba moja kwenye trend.

“Mimi ndio msanii wa rap nadhani nimeongeza namba nyingi kuliko msanii mwingine wa rap. Hii Ni tafsiri kubwa sana kwa muziki wa rap nchini. Muziki wa rap una nguvu Kubwa kuliko wa kuimba japo kuwa marapa wengi wamechoka nadhani wameamua kuikatia tamaa Rap.

“Nadhani wanaweza kujifunza kwa hiki ambacho nimekifanya kwa mwaka huu, muziki wa rap una nguvu sana, sasa hivi tungekua tunatoa tuzo za msanii bora wa mwaka wa rap, sidhani kama nitakosa kila tuzo japo kuwa nafahamu nisingewekwa kwenye vipengele lakini wananchi wangenipa tuzo kwa sababu nilichokifanya kinaonekana,” amesema Rapa Nay wa Mitego.

Leave A Reply