The House of Favourite Newspapers

Mke wa Bobi Wine Ahitimu Masters, Mumewe Amfanyia Sapraizi

0

 

Mwanamuziki na mwanasiasa maarufu kutoka nchini Uganda Robert Kyagulanyi Ssentamu maarufu Bobi Wine, amemuandalia mke wake Barbie Itungo hafla maalum ya kushtukiza baada ya kuhitimu Shahada ya Uzamili ya Haki za Binadamu katika Chuo Kikuu cha London.

 

Bobi amemuandalia mke wake hafla ya kipekee iliyoacha gumzo kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakionesha kuvutiwa na tukio hilo.

“Asante Taata, nakupenda na bila shaka, nitalipiza kisasi hivi karibuni,” ameandika mke wa mwanasiasa huyo, Barbie kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook⁣ .

 

 

 

 

 

Leave A Reply