The House of Favourite Newspapers

Ndege ya Marekani Yadondosha Mabaki ya Injini

0

 

NDEGE ya Boeing ililazimika kudondosha mabaki ya injini yake katika eneo la makazi mjini Denver, Marekani, baada ya injini yake kukumbwa na hitilafu ya kiufundi wakati wa kupaa.

 

 

Ndege hiyo ya Boeing 777, iliyokuwa na abiria 231 na wafanyakazi 10, ilifanikiwa kutua salama katika uwanja wa ndege wa Denver. Hakuna majeruhi walioripotiwa.

 

Polisi katika mji wa Broomfield waliweka mtandaoni picha zinazoonekana kuwa mabati ya sehemu ya mbele inayofunika injini katika bustani ya nyumba moja.

 

 

Abiria waliokuwa katika ndege hiyo walielezea kuwa “walisikia mlipuko mkubwa” mara baada y andege kupaa angani.

 

 

Ndege hiyo yenye nambari ya usajili 328, inayomilikiwa na shirika la ndege la United ilikuwa safarini kuelekea Honolulu, pale injini yake ya upande wa kulia ilipokumbwa na hitilafu, mamlaka ya usafiri wa angani ya nchini Marekani (FAA) imesema.

 

 

Mmoja wa abiria aliyekuwa ndani ya ndege hiyo ameiambia shirika la habari la AP kwamba rubani alikuwa akitoa tangazo wakati mlipuko mkubwa ulisikika.

 

 

“Ndege ilianza kuyumba vikali, mara ikaanza kushuka chini,” David Delucia alisema. Aliongeza kuwa yeye na mke wake waliweka stakabadhi za utambulisha mfukoni “ili ndege ikianguka, tuweze kutambuliwa.”

 

Picha zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha moshi ukifuka kutoka kwenye injini ya ndege hiyo. Moja ya video inayodaiwa kunaswa kutoka ndani ya ndege hiyo inaonyesha injini ikiwaka.

 

 

Leave A Reply