Ngorongoro Heroes Vitani Leo

TIMU ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, leo Jumanne inatarajiwa kushuka dimbani kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi C dhdi ya Ghana kwenye michuano ya AFCON U20 inayofanyika nchini Mauritania.

 

Ngorongoro Heroes inashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza, ikiwa imepangwa sambamba na Gambia na Morocco.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Mkuu wa Ngorongoro Heroes, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, amesema: “maandalizi kuelekea mchezo wetu yamekamilika kwa asilimia kubwa, tulitumia mikanda ya video kuwasoma wapinzani wetu ili kujua ubora na udhaifu wao uko wapi.

Malengo yetu ni kupambana ili tuweze kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia.”Katika michuano hiyo iliyoanza juzi Jumapili, timu ambazo zitafanikiwa kutinga nusu fainali zitakuwa zimefuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia chini ya miaka 20 inayotarajiwa kufanyika Indonesia.

STORI: HUSSEIN MSOLEKA, DAR

Toa comment