The House of Favourite Newspapers

Nicole: Mrembo Kukosa Mishemishe ni Kashfa

0

NICOLE Joy, ni mmoja wa warembo ambao wamejipatia umaarufu kutokana na maumbo yao, kutokana na maisha aliyokuwa akiyaonesha kwenye mitandao ya kijamii. Watu wengi walikuwa wakipenda kumfuatilia na kujua vitu gani anavyofanya.

 

 

Alikuwa akitupia picha kali, akiwa amevalia smati lakini wakati mwingine akiwa shambani akidai ni mkulima.Baadaye akaanza kushiriki kwenye video mbali za wasanii wa Bongo Fleva ikiwemo ile ya Harmonize, Bed Room.

 

 

Gazeti hili lilipata wakati mzuri wa kufanya mahojiano na mrembo huyo ambaye hivi sasa amejiingiza kwenye Bongo Muvi na anaigiza kwenye Tamthilia ya Huba. Fuatilia mahojiano ya Nicole na RISASI kama ifuatavyo hapa chini:

 

 

Nicole: Asante sana, unajua mwanamke mrembo halafu huna mishemishe ni kashfa.

Risasi: Kwa nini umesema hivyo kwamba ni kashfa?

Nicole: Ndio, sasa mwanamke mzuri, hufanyi kazi watu wanakuelewaje, watakuundia kashfa tu kwa vyovyote vile.

 

 

Risasi: Kwa upande wako kama unavyoonekana msichana mrembo, unafanya nini, ili kukuingizia kipato?

Nicole: Ina maana hujuagi kwamba mimi ni mkulima mzuri tu, nikiingia shambani hujui kama Nicole, nashika jembe vizuri. Nikiingia mtaani unaweza usiamini.

 

 

Risasi: Unadhani mastaa hapa Bongo kwa upande wa wanawake wanajisikiaje wakikuangalia wewe?

Nicole: Najua wengi wanakosa usingizi kwa ajili yangu ila wanachotakiwa kupiga kazi na sio kutamani mtu vitu ambavyo anavyo mwenzao.

 

 

Risasi: Lakini mara nyingi unaoneka unasafiri sehemu mbalimbali, una biashara nyingine unafanya nje ya Tanzania?

Nicole: Hapana. Ninapoenda nje ya nchi ni kwa ajili ya kutembea na kubadilisha hali ya hewa maana kitu ninachokipenda mimi zaidi ni kutembea.

Risasi: Mara nyingi huoenekani sehemu za starehe au hata kuwa na

Leave A Reply