The House of Favourite Newspapers

Nikki wa Pili Aogopa Kufungukia Tuhuma za ‘Unga’

Nikk wa Pili

STORI: ALLY KATALAMBULA | RISASI MCHANGANYIKO| RISASI VIBES

RAPA kutoka Kundi la Weusi, Nikki wa Pili amesema hawezi kufungukia sakata linaloendelea jijini  Dar es Salama la baadhi ya  wasanii kutuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya ‘unga’ kwa sababu bado ni tuhuma.

Akichonga na Risasi Vibes, Nikki wa Pili alisema anashindwa kuzungumzia sakata la wasanii wenzake kutajwa kwenye ishu ya unga kwa kuwa bado ni tuhuma ingawa kwa upande mwingine siyo jambo zuri kwa msanii kutuhumiwa na mambo hayo.

Nikk wa Pili

“Ni jambo baya sana msanii kuingizwa kwenye tuhuma za namna hiyo, nitakuwa na uwanja mkubwa wa kuzungumzia sakata hilo endapo majibu ya tuhuma hizo yatabainika, kwa sasa sina ninachoweza kusema zaidi ya kuwapa pole wasanii wote walioguswa na tatizo hilo,” alisema Nikki wa Pili.

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.