The House of Favourite Newspapers

Nilivyovunja Ndoa Yangu na Shetani – 6

0

ILIPOISHIA:

Nikiwa bado naendelea kunywa pombe kwa fujo, Bantu aliingia na kuja kunipigia magoti mbele yangu kuniomba msamaha.

“Anti Konso naomba unisamehe sirudii tena.”

“Bantu au kwa vile nimeonesha nakupenda ndiyo umeamua kunifanyia upuuzi kama ule?” nilimuuliza huku nikiendelea kulia.

SASA ENDELEA…

“Hapana anti Konso ni shetani, siku zote watu wanatafuta sababu za kututenganisha, ni maneno mengi juu yako nimeyavumilia.”

“Maneno yangu?” nilishtuka kusikia vile.

“Ndiyo Anti Konso.”

“Bantu maneno gani?”

“Eti wanasema kukaa na wewe ni sawa na kujivundika kwa kuwa hata nikikuoa huwezi kuzaa watoto wote umewaua.”

“Nani kakwambia?”

“Nilisikia tu.”

 Mmh! Mbona mapya yaani kumbe kulikuwa na watu wananichimba ni kweli sina kizazi baada ya kukitoa pale nilipotaka kuyafaidi maisha. Hii ilikuja baada ya kutoa mimba zaidi ya nne ambazo kidogo zinitoe roho,  ndipo daktari wangu ambaye ndiye mtaalamu wa kutoa mimba za wake za watu zinazoingia nje ya ndoa na wanafunzi akanishauri nikitoe.

Daktari yule alinipa siri nyingi na za watu wengi mashuhuri au wake za watu mashuhuri ambao si waaminifu kwenye ndoa zao. Ambao wanapopata ujauzito wa nje, hukimbilia kwake na kuichomoa hasa baada ya kuingia  kipimo cha DNA, kimewafanya wanawake wengi wawe roho juu na utoaji wa mimba umeongezeka kwa kiasi kikubwa kwa watu kuhofia ndoa zao.

Pia wanafunzi wengi wa vyuo vikuu, shule za sekondari na hata wa msingi walikuwa wakimiminika kwake kutoa ujauzito. Alikuwa na siri nzito juu ya vigogo wa serikali kutembea na wasichana wadogo bila kinga, ikisha nasa ndipo hukimbia pale kuichoropoa.

Kama kuna siku nilikutana na kisichana cha miaka kumi na moja kilichokuwa darasa la sita shule ya msingi. Kwa kweli sikujua kimefika pale kufanya nini kutokana na umri wake mdogo.Taarifa za kile kibinti ziliniacha mdomo wazi eti kimetoka kuchomoa mimba ya kigogo mmoja mtu mwenye wadhifa mkubwa serikalini na jina nilitajiwa.

Halafu kilichonitisha na kuniacha mdomo wazi eti ile ilikuwa mimba ya tatu kuitoa. Mmh! Ukishangaa ya Musa utayaona ya firauni, mbona hali inatisha, kweli dunia imekaa tenge yaani hata watoto wetu tunapishana nao kutoa mimba.

Daktari wangu alinishauri nifunge kizazi baada ya kuponea kwenye tundu la sindano. Lakini cha ajabu mbona ile ilikuwa siri yangu mimi na daktari wao wamejuaje au ndiyo kazi ya daktari kuuza siri za watu kama anafanya hivyo atakuwa hafai. Vilevile sikushtuka sana kwa vile hata mimi nilipata siri za wenzangu kupitia kwake.

Maneno ya Bantu yaliifanya akili yangu ikae sawa na kujikuta nikimsikiliza vizuri.

“Wewe nani kakwambia?”

“Kuna mama mmoja ambaye naye alinitaka kimapenzi nikamkataa.”

“Wewe ulimuamini?”

“Siwezi kumuamini bila kupata uthibitisho kutoka kwako.”

“Basi Bantu jichunge na watu hao hawakutakii mema.”

Sikuwa na haja kuyakumbusha yaliyopita kwa vile tuhuma yangu ilikuwa mbaya kuliko kufumania. Niliamua kumsamehe kwa kujua kumwacha Bantu wapo watu wanaosubiri kwa hamu ili wamchukue na kunicheka.

Nilirudisha uhusiano na Bantu ambaye kweli alionesha kunielewa tabia za mwanzo zilirudi kitu kilichonipa faraja moyoni na kumpa kila alichotaka ili kuhakikisha  hababaishwi na vishawishi vya nje.

Baada ya kumdhibiti Bantu niliendelea na kurusha roho na wazee wenzangu. Kwa kweli Bantu nilikuwa nimempangia sehemu gani za kwenda ili tusije kutana nikiwa na wazee wenzangu ambao ndiyo wanaonilea mjini.

Siku moja usiku  ilikuwa majira ya  saa nne tukiwa tunajiandaa kulala na kipenzi changu Bantu. Mara nilipigiwa simu ambayo ilikuwa ya bwana wangu mmoja wa Kiarabu, Abdul akinijulisha kuwa ameingia jijini usiku ule na ndege na hayupo tayari kulala peke yake kwa hiyo alinitaka tukawe pamoja.

Itaendelea Risasi Jumamosi

 HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO, BOFYA HAPA ===>https://www.facebook.com/shigongotz/

Leave A Reply